PRAY FRO KENYA (TUSALI KWAAJILI YA KENYA)


Hali inayoendelea nchini Kenya tangu waingie katika kipindi cha uchaguzi wa awali na baadae uchaguzi wa marudio, ambao ulipelekea upande wa muungano wa upinzani (NASA) unaoongozwa na Raila Odinga kujitoa baada ya tume ya uchaguzi kupuuza mapendekezo yao ya kuondolewa baadhi ya watumishi wa tume hiyo kudhaniwa kua walihusika na udukuzi wa matokeo ya uchaguzi wa awali.
Hivyo kumekua na kauli zinazopishana, kutoka upande wa muungano wa upinzani na ule wa chama tawala, pia kumekua na maandamano sehemu mbalimbali za nchi hiyo ya Kenya.
Kubwa zaidi ni hili la kila upande kutaka kuapisha raisi wake (inaashiria hali mbaya) yaani kama ikifanyika hivyo uwepo wa machafuko watu wengi watataabia.
Niwakati maalumu kwetu watanzania, wakenya, wana Afrika mashariki wengine, waafrika na dunia kwa ujumla kuliombea taifa hili la Kenya, Mungu alitetee taifa lake.

Comments