Moja ya kitu kinachowachanganya wengi ni kutambua na
kuchagua kipi kinafaa zaidi, kipi ni bora zaidi kukifanya. Jambo hili moja kwa
moja linahusisha uwezo wa mtu kufanya maamuzi, katika hali halisi maamuzi ni
tendo ambalo tunalifanya kwa mamia kila siku katika maisha ya kila siku
kwamfano nile nini, nivae nini, niende saa ngapi, nimpe nani na mengine mengi
yote hayo ni sehemu za maamuzi ambayo tunayafanya kila siku. Lakini kiuhalisia
zoezi la kufanya maamuzi hua linaumiza sana akili kulingana na hofu ya matokeo
yatakayotokea baada ya maamuzi hivyo kutufanya muda mwingine tushindwe kufanya
maamuzi. Kwamfano, umegundua mpenzi wako ana matatizo fulani ambayo ukimwambia
yanaweza kuanzisha mgogoro ambao ni hatari kwa mahusiano yenu labda baada ya
kumwambia mahusiano yenu yanaweza kuvunjika.
Kuna namna kuu mbili za kushughulika na aina mbali mbali za
ufanyaji maamuzi.
Kwanza, kupima idadi
ya faida na hasara. Njia hii ni maarufu sana na takribani watu wengi
huitumia kufanya maamuzi labda kwa kujua au kutokujua. Yaani unapopata wakati
mgumu wa kuchagua kipi ni bora au njia ipi ni bora, unachotakiwa kufanya ni
kuorodhesha faida na hasara au mazuri na mabaya yanayoweza kutokea katika kila
yale unayopaswa kuchagua moja lililosahihi baada ya kufanya maamuzi. Endapo
orodha ya mambo mazuri (faida) ikiwa ndefu kuliko ya mambo mabaya (hasara) basi
jambo hilo au njia hiyo itakua bora zaidi kuiamua lakini endapo orodha ya mambo
mabaya ikiwa ndefu basi njia hiyo si njema kwako kuifuata au jambo hilo si
salama kulifanya ni bora ukatafuta mbinu nyingine ya kufikia kile unchotaka
kukitengeneza kuliko kung’ang’aniana na hilo jambo au njia.
Pili, kupima muda wa uwepo
wa faida na hasara. Njia hii inahusisha zaidi muda, unapotoa maamuzi
unapaswa kuzingatia muda ambao faida au hasara zitadumu baada ya uamuzi utakao
uchukua. Unapotaka kufanya maamuzi
unatakiwa ujiulize katika kila jambo au njia unazotaka kuchagua. Na unapaswa
ujiulize yafuatayo takribani maswali sita ili uweze kupata jibu sahihi:
1. Je,
kuna faida na hasara gani baada ya dakika kumi?
2. Je,
kuna faida na hasara gani baada ya masaa kumi? 3. Je, kuna faida na hasara gani baada ya siku kumi?
4. Je, kuna faida na hasara gani baada ya wiki kumi?
5. Je, kuna faida na hasara gani baada ya miezi kumi?
6. Je, kuna faida na hasara gani baada ya miaka kumi?
Jambo ambalo litakalokua na faida au njia ambayo itakuyokua na
faida zinazodumu kwa muda mrefu ni bora zaidi bali jambo au njia yenye hasara
zinazodumu kwa muda mrefu zaidi si bora au sahihi kulifuata ni vema ukaachana
nalo na kufanya kitu kingine kabisa kuepusha hasara kubwa. Njia ni nadra sana
kutumika maana watu wengi hupenda kuzingatia mambo yaletayo faida kwa haraka
pasipo kuzngatia kuna hasara ambayo itatokea baadae na kudumu milele. Kwamfano,
kuna watu wapo tayari kufanya kazi katika mazingira hatarishi ili tu apate
kipato kwaajili ya kipindi hiki lakini baadae anapata madhara makubwa ya kiafya
ambayo yatadumu katika maisha yake yote kama kupata ulemavu au kupelekea kifo kabisa.
Ili uweze kufanya maamuzi unapaswa zaidi kuzingatia haya ili
kuepusha ufanyaji wa maamuzi kwa kutegemea hisia za kimwili kama tamaa za
kimwili na ushawishi wa marafiki kundi rika. Kwasababu ni rahisi zaidi
kukubaliana na tamaa za kimwili kama ushawishi wa marafiki kwa sababu uamuzi
wake unagusa moja kwa moja ukaribu wa kimazingira na maisha yako. Pesa na
mahusiano ya kimapenzi ni miongoni mwa mifano ya vitu vyenye uwezo mkubwa wa
kupindisha maamuzi, kuna watu wapo tayari kufanya vitu vyenye hasara kubwa kwao
ili tu wakidhi haja ya tamaa zao za pesa au kimapenzi. Umakini mkubwa
unahitajika katika kufanya maamuzi kwa kuzingatia wingi wa faida na hasara na
namna ambavyo faida au hasara zinaweza kudumu katika maisha yetu, ili muda wote
uwe katika hali salama.
Pia unaweza kujifunza umuhimu wa kuchagua jambo moja au njia moja ya kufuata badala ya kuchagua mambo mengi zaidi kwa kubofya kwenye maandishi ya bluu
CHAGUA MOJA, CHAGUA NJIA MOJA
Aksante, nakaribisha ushauri, maswali na maoni.
Karibu!
#Msanzya_2018
#Mfalme_wa_Michongo
Innocent Leonard
Msanzya

Comments
Post a Comment