Maisha yako yanategemea uumbaji wako. Unanachotakiwa
kukijua ni kwamaba una mambo mengi unayohitaji kuimarisha na kuifanya ili kuwa
ya ajabu (ya tofauti). Ikiwa unafikiri maisha yako hayatoka kwa udhibiti wako,
ni kwa sababu umechagua kuacha udhibiti. Maisha yako yataboresheka wakati
unapofahamu maisha sio kitu cha kuvumilia au kusubiria. Ni uzoefu wa uumbaji
wako mwenyewe. Na uzoefu unapatikana katika kufanya jambo zaidi na zaidi, hata
kama unafanya na hupati mafanikio.
Wiki au siku michache ziliyopita, nimejaribu kuwaonyeshea
watu baadhi ya ishara kwamba wewe nimeanza kuchukua hatua za kufanya vitu
vyenye malengo na mtazmo mkubwa. Hata wewe mudau huu ukiwa unasoma jambo hili
na ume bahatika kutambua kwamba wewe pia una nafasi ya kufanya jambo, kwa
kweli, ni mtu mwenye malengo na mtazamo (mfanikishaji) jumla (na kamwe usihisi
kuwa ni vibaya)
Wakati unapanga mambo yako kufanikiwa, kuna rafiki
ambao hua wanjitokeza pia kukupa ushauri au kuomba msaada kwako. Kwa muda wote
unapojaribu kufuatilia sababu za wao kusaidiwa au yale ambayo wao wanaomba
kusaidiwa kwa namna moja au nyingine yanakua hayana mchango kabisa katika
ukamilishaji wa malengo yako na pia hata kwao hayatawasaidia kukamilisha
malengo yao kivile, lengo kuu ni kufurahishana zaidai. Katika hali hii
unajikuta kwa muda mrefu kuwa una wakati mgumu sana kusema HAPANA, kwakua ni
rafiki ambaye anaomba kibali au msaada, mtu ambaye anataka kufanya kitu ambacho
hutaki kufanya au hata mgeni.
Mimi pia nimekuwa huko. Nilikuwa na wakati mgumu
sana kusema watu hapana, hasa wakati nilipopenda sana. Sikuhitaji kuonekana kama
siwajali au nawakwaza. Nilitaka kila mtu awe na uwezo wa kuniona na kufikiria
kuwa nilikuwa mtu mzuri sana ambaye ajawahi kuwapo kwao. Kwa hiyo nikajikuta nawaambia
ndiyo kila kitu, kama mialiko ya sherehe mbalimbali na kukutana na marafiki
ambapo ni safari ambazo sikuwa na nia yoyote, naweza kusema hizi zilikua ni
neema ambazo zimenisababisha kupoteza uelekeo kwa namna moja au nyingine
kabisa, nimejikuta katika mahusiano na watu ambao kwa hakika sikusagwa nao
kabis. Sikuweza kujua jinsi ya kusema hapana bila kujisikia hatia sana. Na kama
nikisema hapana, mara zote kulifuatana na udhuru mkubwa, kwa kawaida ni uongo
ngumu.
Zaidi, nikiwa chuo kikuu, nilikutana na msichana
ambaye hakuwa na shida katika kusema neno hapana. Yeye hakuhisi wala hakuona
shida au haja ya kutoa udhuru. Kama ikiwa hakutaka kufanya kitu, yeye alisema
tu, "Hapana, mimi sitofanya hilo." Ikiwa hakutaka kwenda mahali
fulani, alikuwa waaminifu, akisema, "La, kwakweli nimechoka sana usiku
huu" au "Hapana, ninahisi tu kama kuwepo tu nyumbani." Sikuwa na
hisia na yeye kwa sababu ya hili. Nilitambua kwamba wakati yeye akisema hapana,
hakuwa na sauti nzuri au ya kutisha kifupi alikua anakatisha tamaa kabisa. Yeye
hakutaka kuonekana kuwa mwenye ubinafsi au kama mtu ambaye huwezi kuzingatia.
Pia hakuwa na sauti kama mfanikishaji, jambo ambalo sikutaka kuwa tena kua nae
karibu katika ufanyaji mambo yangu.
Kwa hivyo, nilijifunza kutoka kwake. Zaidi
tulivyozidi, zaidi nilianza kusema hapana kwa watu pia. Bila hata kutambua hilo,
kwakweli alinifundisha jinsi ya kufanya zaidi ya kile nilitaka badala ya kile watu
mwingine alitaka nifanye. Leo, naweza kusema sina tatizo kubwa la kusema hapana
kwa watu. Bila shaka, mimi kutambua kwamba wakati mwingine unasema ndiyo, hata
kama hutaki. Lakini kwa sehemu kubwa, hakuna hata mmoja wetu anayepaswa kuwa na
shida kubwa kwa kusema "hapana." Ikiwa unafanya tofauti, basi soma
vidokezo hivi 10 kuhusu jinsi ya kusema hapana kwa chochote. Utajisikia vizuri
zaidi wakati utakapofanikisha.
Kuwa waaminifu badala ya kufanya mambo ngumu
Njia pekee niliyokuwa nikisema kuwa hapana ni
wakati nilipofanya kwenye kundi la watu
wa kutoa udhuru mkubwa na kunga uongo kama, "Siwezi, muda huo nakwendea
kwa bibi yangu” na baada ya hapo mimi huenda kfanya mabo yangu mengine. "
Ilikuwa ni jambo la kushagaza sana. Nakushauri sifanye hivyo. Kutunga
visingizio na sababu nyingi sana na udhuru itakufanya kuonekana dhaifu! Na
kuunda uongo ngumu ni kuujiongezea shida kwa sababu muda wote utakua una
wasiwasi juu ya kua kama ukigundulika au kama ulielekeza kitu fulani je
watapata au hawatapata. Ni vema ukatuambia ukweli! Sema kitu kama, "Siwezi
kwenda nje, mimi leo nimechoka sana. Nataka tu kupumzika tu usiku wa leo." Au, "Sitaki kufanya
hivyo mimi sina nia." Kuweka hivyo inafupisha,
ina onekana vizur na rahisi. Ni rahisi kama hiyo tu!
Waheshimu
Unapaswa kuwa waaminifu, lakini hiyo haina maana
unahitaji kuwa waaminifu kikatili. Usiwe kama, "Haki ya Mungu, siwezi kamwe kufanya hivyo!" au
"Wewe, kwa nini napenda kufanya hivyo?" Hiyo ni mbaya na hiyo ndiyo
itafanya watu waweze kufikiri wewe hufanya dharau au hujali. Kama nilivyosema,
rahisi, "Hapana nashukuru," ndiyo njia yako bora ya kuwajibu watu
wanao kupa mwaliko ambao wewe huwezi kuhudhuria. Kumheshimu mtu anayekuomba
ufanye kitu.
Usiombe msamaha sana
Ukisha mwambia au ukishawaambia hapana, usianza
kuomba msamaha kama umekosea sana. Hiyo itakufanya uoneke kuwa na hatia na pia
huenda kumfanya mtu mwingine awe na hasira. Baada ya yote, ikiwa unaomba
msamaha, hiyo inafanya kuwafikiri kwamba labda wanapaswa kuchanganyikiwa kwa
wewe kusema hapana. Nilikuwa nikifanya hivyo wakati wote. Sasa ninakataa kwa
ufupi na rahisi, "Samahani, nimechoka sitakwenda nanyi leo" na kuacha
hiyo. Wakati mwingine, sihisi hata haja ya kusema hivyo.
Jaribu kuhusianisha mambo
Kwamfano,
unakuta rafiki yako anaomba muende kupata dinner mahali fulani, lakini huna hisia
au ungependa kwenda na rafiki tofauti. Unaweza kumjibu kama, "Siwezi usiku
huu, lakini unaonaje tukifanya wiki ijayo?" Au marafiki zako wanataka kutazama
filamu moja, lakini huna. Usipate shida we pendekeza movie unafikiri watapenda
badala yake. Daima unahitaji kua makini unaposema hapana leo, lakini wakati
mwingine unafanya. Sasa hakuna kitu kibaya na hicho. Wewe pekee huwezi kufanya
kila mtu kuwa na furaha, fanya yaliyoyamaana kwako.
Kuwa imara
Wakati wa kusema hapana, ni muhimu sana kuwa imara
katika uamuzi wako kwa mtu yeyote atakayefikiria anaweza kuchukua faida yako na
kukushawishi kufanya kinyume. Lakini kama wewe ni imara tangu mwanzo, hawana
uwezekano mkubwa wa kujaribu kukubadili wewe kufanya kile wanachotaka.
Eleza kama lazima
Ikiwa mtu huyu hatakuacha kukushawishi zaidi ili
ubadilishe akili yako, kwa kutoa maelezo kukuonyesha kuwa ni lazima ufanye
anavyotaka. Hapo utalazimika kutoa maelezo kwa ufupi au kwa kina, ili kusaidia
kuondoa mtazamo mbaya juu yako. Sema, "Nimekuwa na wiki ndefu ya kazi na
nimekuwa bize muda wote hii imenifanya kuchoka sana," au "Nilifanya hivyo
hapo awali na sikunipenda, hivyo sitaki kufanya tena”.
Usihisi hatia
Kuwa ujasiri, usijisikie hatia kuhusu kusema
hapana. Sote tunapaswa kusema hapana wakati mwingine na ingawa wakati mwingi
huonekana kuwa sio yakupendeza sana, hiyo haina maana kuna kitu chochote kibaya
katika hilo. Usijilazimishe kusema ndiyo, kwa sababu unahisi watakuona mbaya.
Hakuna chochote kibaya kwa kumshawishi mtu akubaliane na unachotaka wewe! Ikiwa
unajisikia hatia, hiyo itajionyesha na kisha hata wao pia wanaweza kuhisi kama
unapaswa kujisikia hatia, nadhani hilo unajua?
Usiwekatae tu bila ya kusudi la kufanya hivyo
Kipindi cha nyuma, sikujua jinsi ya kuwaambia watu
hapana, nilifanya hivyo wakati wote, hasa kwa wasichana. Msichana anganiuliza naomba
twende mahali fulani, ingawa sikuwa na nia, nilikua najikuta tu kujisikia vibaya
kusema hapana. Kwa hivyo, nilipenda kusema mambo kama, "Siwezi muda huu wa
leo, unaonaje kesho?" hata ingawa sikuwa na nia ya kufanya hivyo milele.
Nilikuwa nimekuwa na matumaini kwamba kama ningeendelea kuifuta ahadi yake kwa
kuisogeza mbele kila siku, hatimaye atapata kuachana na kunishawishi kibinafsi
peke yake. Hiyo ni maana kua nilikua na uoga wa kusema hapana. Usifanye hivyo!
Ikiwa hutaweza kufanya hivyo, usimwambie ungependa, unatarajia mtu mwingine
atasahau au kudhalrau. Haifanyi kazi kwa njia hiyo. Unapo amua kusema hapana
sema ukionyesha pia kusudi lako la kufanya hivyo, usifiche weka wazi.
Tambua wakati wa kusema ndio
Ingawa ni muhimu kusema hapana wakati mwingine, ni
muhimu pia kujua wakati unapaswa kusema ndiyo. Mara tu unapoanza kusema hapana,
huenda ukajaribu kusema hapana wakati wote, lakini hilo linaweza
kuwatenganisha. Kwa mfano, hua una kwenda kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa rafiki
yako kila mwaka, lakini unaona wazi unapaswa kufanya juhudi kusherehekea. Huna
budi kusema ndiyo kwa mahusiano unayotaka kuendelea, lakini unapaswa kusema
ndiyo katika matukio muhimu unayoalikwa. Fikiria mwenyewe mambo ambayo una
wajibu wa kusema ndiyo na bila kujali.
Endelea na mada nyingine
Mara tu unaposema hapana, sio tu kukaa hapo chini wewe
na akili ukifikiri juu hayo. Endelea na mada nyingine kuashilia kitu
alichokueleza kua sio mpango mkubwa, ukizingatia sababu za msingi kweli sio! Hapo
tu sema, "Naam, shukrani," na kisha kuwa kama, "Basi tunafanyaje
juu ya mtihani huo ujao wa biolojia?" au chochote. Hii inaonyesha kwamba
haipaswi kuwa na hisia mbaya kati ya mmoja wenu.
Aksante!
By Innocent Msanzya
Comments
Post a Comment