JINSI YA KUONGEZA UBUNIFU KAZINI

Ili akili zetu ziweze kufikiri vitu vya kibunifu, tunahitaji kuwa na hali nzuri ya kihisia. Wataalam wa saikolojia waweweka wazi kua utendaji wa ubongo huathiri ubunifu na jinsi tunavyohisi huathiri utendaji wa ubongo. Lakini kwa bahati mbaya, hiyo ni rahisi zaidi kusema kuliko inavyofanyika mahali pa kazi ya leo.
Yafuatayo ni maelezo mafupi ya jinsi ambavyo unaweza kuacha kua na mawazo hafifu au hasi; kama ukizingatia zitakusaidi wewe kujitunza vizuri zaidi kazini na kua mbunifu.
Achana na tabia zinazokupelekea kuharibu kazi, au za kuua kuzingatia kazi, kama kutumia sehemu kubwa ya siku yako (au mwishoni mwa wiki) kwenye mitandao ya kijamii au kufanya mawasiliano yanayokuweka mbali na fikra za kazi yako au kuingijiiza kwwenye vikwazo(mijadala mibaya au matukio mabaya) vinavyoendelea katika jamii kupitia mitandao ya kijamii.
Jitahidi kuchukua muda wa kufikiri na kutafakari. Ukifanikiwa kuachana na tabia zinazokuharibu, ni dhahiri utakua na muda ambao utapumzika bila kufanya kitu, tumia muda hua kufikiri na kutafakari kuhusu kazi yako. Jijengee ujasiri - mazoea ya kutafakari hii husaidia sana linapokuja swala la kusimamia matatizo na utambuzi wa maamuzi sahihi. Katika baadhi ya majarida nimeona mwanachuoni Dan Goleman amekua akitumia neno, “Mindfulness” akimaanisha uwezo wa kuona nini kinachoendelea kutendeka wakati kitu fulani kinatokea na kukaa kimya kabla ya kujibu ni ujuzi muhimu wa kihisia. Kuchunguza kwa makini kumethibitishwa kukuza uwezo wa kuzuia madhara hayo ya haraka ya kihisia. Kama utashindwa kabisa ni vema ukachukua kozi ya kupunguza msongamano wa mawazo yanayo kusababishia upungufu wa uwezo wa akili kufanya ubunifu au kusoma na jaribu mazoezi ya kupumua (Pumzi).

Tumia muda wako mwingi kujifunza, jifunze mambo yatakayokusaidia kukupa mtazamo chanya juu ya kazi yako, jifunze mambo yatakayo kusaidia kuwa mbunifu katika kazi yako. unaweza kujifunza kupitia makongamano, semina na matukio mengine yanayofanana na hayo yanayoendana na kazi unayofanya, soma vitabu, majarida na machapisho mbalimbali yanayoendana kazi yako na yatakayokujengea msingi imara wa kufanya yale unayoyaamini yatakufanya wewe uwe ubunifu zaidi katika eneo ambalo linakuhusu, jitahidi angalau kila siku uwe unapata jambo jipya. Usikubali siku ikaisha bila kujifunza kitu kipya utajikuta baada ya muda fulani una mambo mengi unayoyajua. Kitu cha msingi hakikisha kila utakachojifunza unakifanyia kazi pia.
Acha kuogopa udhaifu wako; Usiruhusu akili yako kutengeneza hofu kuhusu madhaifu yako na kushindwa kwako. Hii inaweza kuwa vigumu sana kwa watu wanaofikiriawanaofanya biashara na mafanikio, lakini kitu cha kuweka kichwani ni kwamba mtu anawezaje kuwa na ubunifu bila kushindwa?. Kifupi haiwezekani kufanikiwa billa kupitia changamoto, ukitakakua mbunifu lazima ujiandae kushindana na madhaifu yako na kushindwa kwako.

Zingatia yanayokupa furaha; Ipe nguvu na ujasiri akili yako kufikiri zaidi kile kinachofanya furaha katika kazi. Hisia nzuri zinazozalishwa unapojisikia kushikamana na madhumuni yako binafsi au shirika na mambo muhimu sana kuhusu kile unachofanya hii itakusaidia kuwa na msingi imara wa ubunifu, hata wakati mambo ni ngumu.

Comments