Katika hali ya kawaida, hakuna kitu kinaumiza kichwa pale
unapokua mtu wa kujitaidi kufanya kila namna ili uweze kusonga mbele lakini kwa bahati mbaya ukawa karibu na
mtu anayelalamika wakati wote na daima unapoomba ushauri ana kitu hasi cha
kusema, kukukatisha tamaa. Ikiwa utaweza, unapaswa kujiweka mbali nae au
kupunguza mawasiliano yako na mtu/watu hao, lakini kama hiyo haiwezekani, labda kwa
kua ni mtu katika mazingira yako kwamfano
ni mfanyakazi wa kushirikiana nae au mwanachama mwenzako, au ni mwanafamilia yako,
inaweza kuwa vigumu kujiweka mbali nae. Katika hali hizo, ni muhimu ikiwa una mbinu
chache, sio tu jinsi ya kujikinga na nguvu zao hasi lakini jinsi ya kugeuza
mawazo yao hasi kua katika mwelekeo mzuri zaidi. Njia moja ya ufanisi zaidi ya
kushawishi mawazo ya mtu mwingine ni kuwaelekeza tena mawazo yao kwa njia ya
hila.
Kile mtu anazungumza au kile anachofikiri kinatokana na kile anachokizingatia
zaidi katika akiri yake. Kuna makundi mawili tu ya vitu ambayo husababisha
hisia katika maisha ambayo unaweza kuzingatia: Mambo unayotaka na mambo ambavyo
hutaki. Kila kitu ambacho unaweza kufikiria kinachosababisha aina yoyote ya
hisia muhimu inaweza kutatuliwa kwenye mojawapo ya makundi hayo mawili.
Mambo usiyoyataka/ vitu vyote ambavyo hutaki: Kuharibika, kupoteza kazi, usaliti,
kifo cha mtu unaye mpenda-vitu.
Mambo nayopenda/ vitu unavyopenda: Wapenzi, marafiki bora, sherehe ya
kuzaliwa, kupandishwa cheo-kila kitu unachotaka.
Labda, sio kitu cha kushangaza, watu ambao wanazungumzia mambo hasi
wakati wote ni watu ambao hisia zao huyazingatia zaidi mambo hayo katika maisha
yao wasiofurahia na hawapendi. Kitu ambacho hawajui ni kwamba kile
wanachokizingatia zaidi katika akiri zao hufanya kazi kwa namna ya kuhamasisha
(anzisha)/ kuzuia, maana yake, unapochunguza vitu visivyofaa, huzuia uwezo wako
wa kuona mambo mazuri (chanya) na unapochunguza zaidi vitu vyenye kufaa vinaanzisha/
vinaamasisha uwezo wako wa kuona mambo mazuri(chanya). Hii ina maana kwamba watu ambao hutumia kiasi
kikubwa cha muda wao kuzingatia vitu visivyohitajika katika maisha kukamatwa
kwenye ufuatiliaji wa vitu au mabo ya kipuuzi ambayo ni vigumu sana kuachana
nayo kwa sababu ubongo wao umefuta chanya.
Hii ni ya maana kwao, lakini ikiwa unapaswa kuwa karibu nao kwa muda mrefu,
basi ni ya maana kwako pia. Habari njema ni kwamba kile akili inakizingatia
zaidi hakiondoki haraka lakini huondoka kwa haraka zaidi pale watu wanapo
zingatia mambo mazuri ya kihisia yenye faida wakati wanapokua wanazingatia pia masuala
mengine zaidi ya maisha yao. Kwahiyo hapa
wanachohitaji ni msaada mdogo kutoka kwa wewe ili kuvunja/kuzuia mzunguko wa mambo
hasi katika akili zao na kuwasaidia kufanya mabadiliko. Mambo unayotakiwa
kufanya ili uweze kuwasaidia kuzungumza juu ya mambo chanya ni kuelekeza mawazo
yao kwa kitu wanachotaka kufanya/ mambo
wanayohitaji.
Utakapo kua unajaribu kufanya mabadiliko wakati ubongo wa mtu huyo umekwama
kwenye mambo yasiofaa na wakati huo wewe ndo unajaribu kuelekeza mawazo yao kua
katika mtazamo chanya, kwa awali, utaona wazi hawatakuwa na uwezo wa kufikiria
kitu chanya, wanaweza kukupa nafasi tupu / au wataweza kurudi nyuma kwenye
mkondo wao wa kufikiri mambo hasi.
Kwamfano soma mazungumzo haya:
Rafiki: Mimi sipendezwi na vile ambazo mume
wangu ananifanyia, hajawahi nifanyia kitu kizuri.
Wewe: Inaonekana kama wewe umekasirika sana. Licha ya hayo uanyolalamika
kakufanya lakini lazima kuna wakati mwingine yeye alikufanyia mzuri?
Rafiki: Sio kweli. Hivi karibuni, yote anayofanya ni chukizo kwangu.
Unaweza kuona jinsi ambavyo kipindi cha wawali unapojaribu kutengeneza
mtazamo chanya, lakini mtu huyo akakurujirudisha tena kwenye ule mkondo wake wa
fikira hasi. Ukiona hali ipo hivyo usiachie hapo endelea kujaribu kumbadili. Inaweza
kuchukua majaribio kadhaa ili kuelekeza mawazo ya mtu katika kitu fulani anachotaka
katika maisha yake lakini mara tu wanapotimiza hili, kutakuwa na mabadiliko ya
kihisia hata kama ni mafupi. Inaweza kusaidia kutoa maoni.
Wewe: Je! Unakumbuka kuhusu mwishoni mwa wiki iliyopita alipokupa zawadi na
kukuchukua kwa chakula cha jioni?
Rafiki: Ndiyo, hiyo ilikuwa nzuri (Badiliko la muda kugeuka kuelekea kwenye
mambo anayoyataka) ... lakini haifanyi mambo mazuri kwa vitu vingine (anarudi
kwenye mambo yasiyohitajika).
Ikiwa mada yake inahusisha mambo yasiyofa kabisa, unaweza kusaidia
kubadilisha somo kabisa.
Wewe: Kwa kawaida mahusiano yoyote huwa yanakua imara na kunawakati yanakua
pungufu, basi tupange safari ya kupoteza mawazo ili tutoke. Ungependelea kwenda
wapi?
Rafiki: Mimi hakika ninahitaji tupange siku ya kuogelea. Ningefanya masaji ningejisikia
vizuri sana. Ninafurahi kuwa na rafiki mzuri kama wewe.
Unapowahimiza na kuwafariji mtu kuelekeza mawazo yao katika mambo mengi
yanayotahitajika katika maisha yao, angalia mabadiliko katika sura zao za uso
na lugha ya vitendo vya mwili. Watu wanapoanza kuzungumza juu ya matukio mazuri
ambayo wanajisikia vizuri, huanza kutabasamu au kucheka; ni jambo la kihisia
linaloonyesha akili zao kujihusisha na mambio chanya. Wao watahisi vizuri na wewe
pia utahisi hivyo.


Comments
Post a Comment