Kusimamia fedha zako binafsi ni
mchakato unaoanza na kujua hali yako ya kifedha ya sasa; mchakato unaendelea na
kuanzishwa na kuzingatia malengo yako, ili uweze kuendeleza mikakati ambayo
itawawezesha kupata kutoka kwa hali yako ya sasa ili kufikia malengo yako. Upo
usemi wa Kiswahili unaosema mtoto halali na hela. Umewahi kuuelewa
vizuri? Kama bado, basi hiyo ndiyo inasababisha changamoto zako kifedha.
Mtoto
halali na hela kwa sababu mtoto akipata hela hana siri, atamwambia kila
mtu, atamringishia kila mtu, na wakati wote, atashika hela yake kwenye
mkono wake. Sasa ukitaka kuipata fedha ya mtoto huyo, subiri alale,
utaichukua kirahisi tu, na akiamka wala hatakuwa na kumbukumbu fedha
hiyo imeenda wapi.
Hivi
ndivyo watu wazima wengi wenye changamoto za fedha wanavyoishi.
Wakipata fedha, iwe wamepokea mshahara, au wamepata faida, basi kila mtu
atajua huyu ana fedha. Wataanza kutoa zawadi zisizo za msingi, wataanza
kutoa ofa za vinywaji kwa watu, mtu atakutana na muuza nguo, hakuwa na
mpango wa kununua nguo ila kwa kuwa amemuona na fedha anayo, basi
ananunua.
Sasa
jamii inapojua mtu ana fedha, na anazitoa kirahisi, kila mtu anatafuta
mbinu ya kupata fedha hizo. Hapo sasa ndiyo utaona kila mtu anakuja na
shida yake, shida ambayo kwa namna inaelezewa, utaona ni kubwa sana na
wanahitaji msaada wako wa fedha, na kwa kuwa kila mtu anajua una fedha,
basi huna budi bali kuchangia.
Hata
matapeli wa fedha pia, wanafuata wale ambao wanaonekana wazi kwamba
wana fedha, na wanakwenda na mitego ambayo ni vigumu kwa mtu kuing’amua.
Hivyo
rafiki, hatua ya kwanza ya kutuliza fedha zako, acha utoto kwenye
fedha, acha kuionesha dunia kwamba umepata fedha. Yaani kama kwa matendo
yako tu mtu wa nje anaweza kujua una fedha au huna, wewe bado una tabia
za kitoto kwenye fedha.
Jifunze nidhamu ya fedha jambo kubwa la kuzingatia ili uwe na nidhamu ya
fedha binafsi au katika hatua ya kifamilia ni kuhakikisha unakua na bajeti na kuifuata. Kwamfano katika hatua ya undaaji bajeti kifamilia, si lazima kuwa
na mshahara mkubwa kuwa bali ni kua tu nia ya kuendeleza ufanisi wa utekelezaji
mambo ya kifamilia kwa kuzingatia vipaumbele kulingana na upatikanaji wa fedha
(kipato). Kuna watu binafsi au familia nyingi zinafikiri kwamba bajeti sio kitu
cha lazima sana kwao kwa sababu wao wana chanzo cha kawaida cha mapato na
gharama zao za kila mwezi ni mfano wa familia yoyote ya wastani, kama kulipa
kodi, bili za huduma, shule za watoto, au gharama za gari. Bila kujali uwepo wa
bajeti katika uchumi wa familia, unasaidia kutafakari njia za kipato, inaweka
wazi uwezo wa kipato, kuonyesha vipaumbele wa matumizi ya kipato, kusukuma
utekelezaji huku na kutoa tahadhari. Hivyo unahitaji kuandaa bajeti yako
binafsi au ya familia. Pia
jijengee
ukomavu kwenye fedha, ukomavu ambao ukiwa na fedha au ukiwa huna hakuna
mabadiliko kwenye tabia. Hiyo itakuwezesha kutulia na fedha ambazo
unazipata na kujiepusha na wanyonyaji wa fedha wanaokuzunguka.
Nakaribisha maswali na maoni.
Karibuni sana!
#Msanzya_2018
#Mfalme_wa_Michongo
Comments
Post a Comment