CHAGUA MOJA, CHAGUA NJIA MOJA



Ufanisi unapatikana kwa kutokuwepo kwa makosa. Kadri unavyopunguza utokeaji wa makosa unaongeza ufanisi. Kulingana na maandiko matakatifu na taarifa mabalimbali za kitaalamu wanathibitisha kwamba binadamu ni dhaifu katika namna moja au nyingine, hivyo kutokea kwa makosa katika utendaji wake ni hali ya kawaida, ingawa kuna uwezekano mkubwa wa kuepuka makosa ni finyu sana. Hivyo ukweli ni kwamba ili binadamu aweze kuepuka makosa katika ufanyaji mambo yake anahitaji uwepo (utulivu wa akili na kuiweka akili yake yote katika jambo au kitu tu anachokifanya wakati huo).

Kwa kuzingatia ukweli huu ni ni dhahili unapaswa kua na kitu kimoja pekee cha kufanya, kwaajili ya kuboresha au kuimarisha ufanisi katika ufanyaji mambo, hivyo ni vema zaidi au inapendeza zaidi na ina manufaa zaidi katika ufanisi endapo ukichagua jambo moja tu, kitu kimoja tu au njia moja tu ili uifanyie kazi (kulipa uwepo). Kulipa uwepo jambo moja inamaanisha kusahau mengine yaliyopo na kuamini kua hayapo bali upo na jambo hilo moja tu.

Ukichagua jambo moja au kitu pekee cha kufanya unaongeza ufanisi, ufanisi ukiongezeka utafanikiwa zaidi kuliko ukachagua mambo mawili au zaidi mbayo ni mengi na itakupa kazi kuyapa uwepo yote kwapamoja, hivyo mwisho wa siku mambo yote yatakushinda. Msemo wa Kiswahili unaosema “Mshika mbili, moja humponyoka” unathibitisha jambo hili kwamba kama ukipendelea zaidi kufanya mambo mawili au zaidi kwa wakati mmoja lazima itafika hatua utashika jambo moja na mengine yatakushinda, yaani huwezi kushika mambo mawili kwa wakati mmoja “Mafahari wawili, hawakai zizi moja” mambo mawili au zaidi huwezi kuyaweka katika akili moja kwa wakati mmoja, lazima moja litasahaulika ili moja libaki.

Ili ufanikiwe katika hili, unahitaji kufanya maamuzi. Na uwezo wa kufanya maamuzi ndicho kitu cha pekee kabisa unachopaswa kua nacho wakati wa kufanya chaguzi (kuchagua) maana ndiyo msingi mkuu wakukupatia njia sahihi ya kufuata, au jambo sahihi na bora zaidi la kusafanya maana si kila njia au jambo nisahihi au linafaa kufanya pia kila njia au jambo linapishana ubora kati ya njia au jambo moja na jingine.  Pia uwezo wa maamuzi ndio mtaji wa ufanyaji jambo, kitu au kufuata njia uliyoichagua. Hivyo unapaswa kuchagua jambo lililosahihi na bora zaidi kuliko yote ndilo ufanye na ufanye au njia bora zaidi ya kufuata na uifuate.

Pia unaweza kujifunza jinsi ya kutambua jambo au njia sahihi kwa kubofya  kwenye maandishi ya bluu. JINSI YA KUTAMBUA JAMBO AU NJIA BORA NA SAHIHI

Aksante, nakaribisha ushauri, maswali na maoni.
Karibu!


#Msanzya_2018
#Mfalme_wa_Michongo
Innocent Leonard Msanzya

Comments