Dunia ingekua yenyewe tu kusingekua
na tatizo, lakini ulimwengu ndiyo unaokusanya uwepo watu na matatizo
yake. Hapa ndipo watu tunapoanza kuangaika kushughulika na kumaliza
matatizo lakini cha kustaajabisha ni kwamba, kadri watu wanavyoshugulika
kutatua matatizo wazazidi kutengeneza matatizo zaidi. Sio rahisi kelewa
kwa haraka ila ngoja tujaribu kuangalia mifano ifuatayo:
Hili halina ubishi kua maisha ni magumu, Lakini wanaosema maisha magumu nadhani
wanamaanisha hawana fedha za kutosha kuendeshea maisha yao ya kila
siku. Lakini katika uhalisia ukiwaza unagundua kua maneno haya yanasemwa
bila kuzingatia kwamba kuna matatizo ya kutokuwa na fedha, halafu kuna
matatizo ya kuwa na fedha. Na haya ni matatizo tofauti kabisa. Hivyo
kama hukuwa na fedha na ukawa na matatizo, na ukizipata fedha siyo
kwamba matatizo yataisha, bali litaondoka la kutokua na fedha na kuja
matatizo ya fedha. Siwezi kumlaumu aliyegundua fedha.
Ni dhahili kwamba kutembea kwa miguu ni kazi, Lakini wanaosema kutembea kwa miguu ni kazi nadhani wanamanisha hawawezi kuhimili kutemebea umbali mrefu kwa miguu. Lakini katika uhalisia ukitafakari kwa kina utagundua kua kuna kutokuzingatia matatizo yaliyopo katika njia nyingine za usafiri, kutembea kwa miguu ni tatizo, halafu kuna matatizo ya kutumia au kumiliki usafiri kama gari. Hivyo kama ukiwa huna gari katika safari ndefu ni tatizo, na kwamba ukipata gari haimaanishi kwamba matatizo yataisha, bali litaondoka la kutembea kwa miguu na kuja matatizo ya gari. Siwezi kumlaumu aliyebuni gari.
Ni kweli kabisa kutokua na mme au mke ni shida. Lakini wanaosema kutokuoa au kutokuolewa ni shida wengi wao wanamaanisha maisha yao hayawezi kua salama au kamilifu bila kua na mke au mme. Na ukitafakari utagundua kua kiuhalisia kuna tatizo la kutokua na mke au mme alafu kuna matatizo ya kua na mke au mme. Haya ni matatizo tofauti kabisa. Hivyo naweza kusema kua kutokuoa au kuolewa ni tatizo, na ukimpata mke au mme haimaanishi kwamba matatizo yataisha bali linaondoka tatizo la kutokua na mke, yanakuja matatizo ya mke au mme. Siwezi kumlaumu aliyewaumba mtu mke na mme.
Kulingana na Joseph Satalin alisema " Kifo ndio suluhisho la matatizo yote" hivyo kama unaishi tegemea kukutana na matatizo tu, hakuna namna ambayo unaweza kuepuka kukutana na matatizo hapa duniani.
Death is the solution to all problems. No man - no problem.
Joseph Stalin
Read more at: https://www.brainyquote.com/topics/problem
Read more at: https://www.brainyquote.com/topics/problem
Death is the solution to all problems. No man - no problem.
Joseph Stalin
Read more at: https://www.brainyquote.com/topics/problem
Yapo mengi yakuelezea lakini kwa hayo machache ni matumaini
yangu kua umepata kitu fulani tayari, ni kweli kutafuta suluhisho la matatizo ni kazi kubwa, lakini lazima tuendelee kuifanya kwakua tumezaliwa ili kutatatua matatizo na si kutengeneza matatizo, hivyo kama binadamu aliyekamilika lazima kila siku uwe makini kufikiri njia za kutatua matatizo yanayokuzunguka, kitu kikubwa cha kuzingatia
kuyachukua matatizo kama changamoto ili uzidi kuchukua hatua zaidi za
kufanikisha malengo uliyonayo hapa duniani, maana changamoto ni sehemu
ya maisha yetu ya kila siku. Na dunia haikosi changamoto za kutupatia
mpaka ile siku ambayo tunaondoka hapa duniani. Hivyo kukimbia changamoto
yoyote unayokutana nayo ni kujidanganya, kwa sababu hazitakuacha.Read more at: https://www.brainyquote.com/topics/problem
Nakaribisha ushauri na maoni.
#Msanzya_2018
#Mfalme_wa_Michongo
Innocent Leonard Msanzya
Comments
Post a Comment