FANYA KAZI UKIWA NA TUMAINI LA MAFANIKIO.

Mafanikio sio kitu ambacho hua kinatokea kwa bahati mbaya, ili kuwa na tumaini la mafanikio kupatikana lazima ujifunze kua na mipango madhubuti ya kufanikiwa na uthubutu mtiifu wa kuchukua hatua kadhaa kuelekea kijiji cha mafanikio, achana na tabia ya kufanya kazi tu bila kujua lini au saa ngapi utafanikiwa.
Ili kufanikiwa lazima pia uweke/utengeneze mazingira ya kufanikiwa, ambapo ili uwe na uhakika wa kufanikiwa katika jambo unalolifanya inategemea misingi ambayo umejiwekea, ambayo ni kama ifuatayo:
1. KUSALI- Tambua umuhimu na msaada wa imani katika kufanikiwa kwako.
2. KUA NA RATIBA NA MIPANGO YA MAENDELEO- Hakikisha una ratiba ya kukuelekeza muda na ukomo wa kufanya mambo yako lakini pia mipango na madhubuti na mikakati makini itakayo kufanya ufikie mafanikio uuyatakayo. Unahitaji ubunifu mkubwa katika kutimiza hatua hii, ili uweze kupanga mipango yenye kuendana na uwezo wako.

Kama unahisi kupungukiwa hali ya ubunifu bonyeza hapa kujifunza zaidi jinsi ya kuongeza ubunifu JINSI YA KUONGEZA UBUNIFU KAZINI

3. HESHIMU MUDA, MIPANGO NA RATIBA YAKO- Heshimu ratiba na mipango uliyojiwekea kwa kuhakikisha unafanya kila ulichopanga kwa wakati.
4. KUPENDA UNACHOKIFANYA- Penda mipango yako, penda kazi unayofanya ili kukuongezea msukumo wa ndani wa ufanyaji kazi..itakusaidia kufanya kwa bidii bila kuchoka na muda wote utatamani uwe kazini.
5. KUJIAMINI- Amini kua maamuzi yako na unachokifanya ni sahihi, usifuate maneno au mawazo ya mtu mwingine.
6. KUJITUMA- Fanya kazi kwa bidii, akiri na kwa nguvu zako zote.
7. KUA NA DHAMIRA YA KWELI-Kua na dhamira ya kweli kuhusu kufanikiwa na mafanikio yako, hakikisha unadhamiria kutoka moyoni kufanikiwa kwa namna au hali yoyote ile.
Aksante, nikutakie mafanikio mema na karibu tena!

Comments