Kushukuru ni kuonyesha kutambua umuhimu wa kile ulichopata na umuhimu wa yule aliye kupatia kile kitu ile hali. Kushukuru kunatengeneza njia ya kupata tena au kupata zaidi. Haijalishi umepata kitu, hali fulani, umepata kidogo au umekosa kabisa, unachotakiwa kufanya kwa haraka na kwa dhati kabisa ni shukuru, hii itakutengenezea njia ya kupewa zaidi na zaidi au kama hujapata itakutengenezea mazingira ya kupata katika awamu zijazo au pale kitakapopataikana unachohitaji. Katika hali ya kawaida unaweza kumfanyia kitu mtu unayempenda (rafiki, ndugu, mzazi au jamaa tu) ukiwa na dhamiri njema kabisa ya
kuonyesha UPENDO wako kwake, kwa kawaida ni nadra sana kwa unaemtendea
kuitambua dhamira yako na kulichukulia kwa uzito wa dhamira sawa.
Kwanini watu wengi ni wagumu kushukuru?
Uwepo wa kundi kubwa la watu wasioshukuru, pale wanapopata au wanapokosa kile wanachokihitaji unatokana na kutokutambua dhamira ya utoaji, au dhamira ya dhati kutoka kwa mtoaji. Mtoaji hua anatoa kile anachotoa akidhamiria kwa dhati mpokeaji atapendezwa na utafurahia kile atakachotoa, hua inatengeneza mazingira tofauti pale mpokeaji anapoonyesha utofauti hisia katika kupokea au baada ya kupokea.
Aina za watu au makundi ya namna ya upokeaji (Ndugu, rafiki au mzazi); Kuna takribani makundi matano ya watu katika kutambua dhamira ya utoaji na namna ya upokeaji hali au kitu kutoka kwa mtu mwingine.
Aina za watu au makundi ya namna ya upokeaji (Ndugu, rafiki au mzazi); Kuna takribani makundi matano ya watu katika kutambua dhamira ya utoaji na namna ya upokeaji hali au kitu kutoka kwa mtu mwingine.
1. Anayeelewa sawa sawa na dhamira yako..huyu atasema aksante na
atajitahidi kutafuta namna ya kurudisha fadhila na hata kama atashindwa kabisa
atakuombea baraka kwa Mungu.
2. Analeyeelewa lakini si sawa na
uzito wa dhamira uliyoiweka ndani yako wakati kwasababu tayari kuna mtu
au watu wanaomfanyia sawa au zaidi ya umevyomfanyia wewe. Huyu atasema
aksante tu.
3. Anaelewa na lakini hajishughulishi kufukiri
dhamira yako nini kwasababu ulichokifanya tayari anacho au anafanyiwa
sana na haitaji zaidi. Huyu ata aksante sio rahisi kuitoa na kuipata
kwake mpaka umkumbushe vipi mbona kimya.
4. Hasiye elewa. Hata
umfanyie nini huyu mtu hataridhika/hatosheki kwahiyo hasemi aksante
wala nini zaidi atakwambia hii ndio umeona unipe mimi? au haka tu? sasa
hii inafaa kufanyia nini?.
5. Hasiye elewa kabisa. Hatari kweli
hapa, mtu huyu haelewi kabisa na atakuchukulia katika mtazamo hasi.
Badala ya kushukuru atakutukana sana hadi utajuta kumfanyia huo
mwema/upendo wako. Atakulaani badala ya kukubariki.
Namna ya kutengeneza mazingira endelevu ya kushukuru
Namna ya kutengeneza mazingira endelevu ya kushukuru
Comments
Post a Comment