Katika hali ya kawaida kama tulivyoona katika chapisho la "Kwanini watu wengi watu wanashindwa kushukuru? kama bado hujasoma unaweza kusoma kwa kubonyeza hapa kwenye maandishi ya bluu Kwanini watu wengi ni wagumu kushukuru? kua watu wengi
wanashindwa kutoa shukurani zao kwa watu wanaowajali pale wanapopata au
wanapokosa kile wanachokihitaji.
Katika familia: Ni rahisi sana kuona katika hadhi ya kifamilia
baba, mama watoto na hata ndugu wengine, kila mmoja haoni haja ya kumshukuru mwingine. Lakini ili kujenga mahusiano mema kila mmoja anatakiwa kumshukuru
mwingine. Watoto wanaapaswa kuwashukuru wazazi wao kwa kuhakikisha wanasema asante kila wanapopata chochote kiutoka kwa wazazi wao, lakini pia kwa kuwajibika katika kazi mbalimbali za kifamilia zinazowakabiri wazazi wao zilizo ndani ya uwezo wao kama watoto. Ni kweli mzazi anapaswa kuhakikisha familia inakua na chakula muda wote, lakini pia kama pesa nyumbni ipo lakini chakula hakuna mtoto anaweza kuwajibika kwenda sokoni kufuata chakula cha familia, kama chakula kipo lakini hakijapikwa watoto pia wanaweza kupika chakula, nyumba ikiwa chafu wanaweza kufanya usafi wa nyumba lakini hii haipo sambamba katika kila familia inategemea zaidi mazingira ya familia pia. Katika familia si watoto pekee ndio wanapaswa kuwashukuru wazazi, maana tumezoea tu kuona watoto ndio wanapaswa kuwashukuru
wazazi wao, lakini wazazi pia wanapasa pia kuwashukuru watoto wao, wazazi wanaweza kuwapa zawadi watoto wao katika kile wanachofanya, kama zawadi hakuna, wazazi wajribu japo kuonyesha utambuzi wa kile kilichofanyka kwa vitendo au maneno yenye hisia za kutoa hamasa kwa watoto wao. Kama mzazi ni mtu mwenye kipato kilichopangiliwa vizuri anaweza kuweka mpango wa kutoka na familia (watoto) kwenda mapumziko ya mwisho wa wiki, mwezi au mwaka ili kuwajengea watoto na familia uwezo wa kuwajibika zaidi.
Katika kazi: Kazini pia kama wewe ni kiongozi au msimamizi
Kwanza shirikisha, jitahidi kuwaweka wazi wafanyakzi wako kile unachokipenda waao wakitekeleze, ukifanya hivyo utawafanya wafanyakazi wajisikie huru kufanya majukumu yao na kua wao pia wanathamani katika ofisi na unatambua uwepo wao na juhudi zao.
Pili fahamu wafanyakazi, jitahidi kufahamu mambo
ambayo wafanyakazi wako wanayapenda, hii itakusaidia katika mgawanyo wa majukumu na pia hata katika kutoaji wa zawadi kwa wafanya kazi. Kutoa zawadi ni namna ya wazi na ya kawaida kabisa tuliyoizoea ya kuonyesha shukrani na kutambua uthamani kwa wafanyakazi na kuhamasiha hali ya kufanya kazi kwa wafanyakazi wako siku hadi siku tofauti na kuonyesha
kua unawajali. Katika kutoa zawadi kama huwezi kupangilia zawadi kulingana na hisia za yale wanayoyapenda inashauriwa kua ni vema ukatoa zawadi katika mfumo wa pesa kama unaweza kutoa pesa kwa wafanyakazi wako,
unaweza kutoa kama vile mwisho wa mwaka kutoa bonasi pamoja, ikishindikana kabisa ni vema ukatoa tu hata cheti cha kuonyesha
kuwa unatambua juhudi zao katika kufanikisha malengo ya kampuni na unajali kuwapo kwao katika majukumu yao ya kiofisi.
Tatu mapomziko, weka katika ofisi yako utaratibu wa kutoa mapumziko kwa wafanyakazi wako, kama kila siku, mwisho wa wiki na katika siku za sikukuu kila inapoonekana uwezekano wa kufanya hivyo. Kuna wakati mambo yanaenda ndivyo sivyo siku ya kupumzika kunakua kunashughuli muhimu ya kufanya, inashauliwa kama siku hiyo haitawezekana tafuta siku nyingine
utayowapa wafanyakazi wako mapumziko.
Nne, chakula cha pamoja (Lunch or Dinner). inasemakana kua chakula ni zawadi nzuri zaidi na inayosaidia kutengeneza mahusiano bora kati ya wafanyakazi. Kila mmoja anafurahia chakula. Hivyo
wakaribishe chakula cha pamoja mchana au cha usiku wafanyakazi wako au hasa zaidi katika sikukuu za
kuzaliwa au matukio muhimu katika mwaka au bila kuwepo kwa sababu yoyote
ile, katika kufanya haya unakua umetoa muda wa kufanya mazungumzo kirafiki zaidi, katika mazingira haya ndipo wafanyakazi wako wataweza kukwambia hata mambo ambayo wao hawayapendi au wanayapenda kirafiki (kiutani utani) na kupumzisha akiri na kutengeneza akiri mpya pia (refreshment).
Tano, nafasi za mafunzo, kama msimamizi au kiongozi unaweza kuweka utaratibu rasmi wakutoa nafasi za mafunzo, mara nyingi wafanyakazi mafunzo ya mara kwa mara kuhuwisha uwezo wao na hali yao ya ufanyaji kazi hivyo wanahitaji nafasi kwa ajili ya mafunzo zaidi. Wapatie fursa za kushiriki matukio
mbalimbali ambayo wanavyopendelea na vinayoweza kuwasaidia katika utekelezaji wa malengo ya ofisi na kazi zao pia.
Haya ni baadhi ya mambo muhimu sana ambayo huongeza umoja, ushirikiano pamoja na uzalishaji katika kampuni au shirika lako, haya si mambo ya kupuuzia kama kiongozi usiache kuyafanya bila sababu za msingi ambazo wafanyakazzi wako hawazielewi.
Lakini pia kama mfanyakazi, sio kampuni au viongozi tu ndio wanastahili kuwashukuru wafanyakazi. Bali kama mfanya kazi pia unatakiwa kuonyesha shukurani zako kwa ofisi na kiongozi wako kwa kuhakikisha unajituma zaidi, na kushiriki zaidi katika utatuzi wa matatizo mbalimbali yananyoikabiri ofisi au kutekelza kwa bidii na kujitoa kutekeleza majukumu yaliyo katika kazi yako. Kama mfanyakazi unahitaji kujifunza mbinu zitakazo kufanya uwe mbunifu kazini. Bonyeza maandishi ya bluu kujifunza zaidi.
JINSI YA KUONGEZA UBUNIFU KAZINI
JINSI YA KUONGEZA UBUNIFU KAZINI
Katibu tena.
Comments
Post a Comment